Hawa ndio wezi sugu ambao wamekuwa wakiwaibia wakazi wa Kitengela, Ruiru na Ngong

- Wezi wanne walikamatwa Jumatano Agosti 1, mtaani Athi River mjini Nairobi na nyuso zao kuanikwa na maafisa wa polisi ili kila mwananchi aweze kujitahadhari na wao

-Inaonekana serikali sasa imebuni mbinu mpya ya kukabiliana na wahalifu hasa ya kuanika nyuso zao mitandaoni

Washukiwa wanne wa wizi walikamatwa mtaani Athi - River kwa madai kuwa wamekuwa wakiwahangaisha wananchi kwa kuwaibia mali zao hasa vifaa vya kieletroniki ikiwemo televisheni , redio nakadhalika

Habari Nyingine : Mwanamke akutwa akiiba mtaani, arekodiwa kwenye video akipata kichapo cha mbwa koko

Habari Nyingine : Vera Sidika na Otile Brown wabainisha kuwa hawajatengana, watoa video

Wanne hao walikiri kwamba wao huiba katika mitaa za Ruiru, Kitengela, Juja na kwenye nyumba zilizoko katika barabara kuu ya Ngong.

Vifunguo kadhaa vilipatikana na gari nyeusi la aina Toyota lenye nambari ya usajili KBT 023 Q wakati maafisa wa polisi walipokuwa wakifanya msako.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Wezi hao ambao nyuso na majina yao yameanikwa kwenye mitandao ya kijamii wamezuiliwa katika kituo cha polisi cha Athi River.

Habari Nyingine : Bili ya stima ya Jeff Koinange kila mwezi yawaduwaza Wakenya

Inaonekana maafisa wa polisi wamebuni mbini mpya ya kukabiliana na wezi ambapo wanaanika nyuso zao kama njia moja ya kuwatahadharisha wananchi kuhusu wezi wa aina hiyo.

Alhamisi Julai 26, maafisa wa polisi pia walianika nyuso za washukiwa 2 wa ujambazi ambao wamekuwa wakiwapokonywa wananchi bidhaa zao kwenye mitaa ya jiji la Nairobi.

Kompyuta kadhaa zilinaswa baada ya maafisa kufanya msako na inasemekana mtu mmoja aliweza kupata kompyuta yake kwenye kuompyuta hizo zilizokuwa zimeibwa.

Read: ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibX52fpFmn5qvkWK7pbXOZq6espliwLaz1GaYppqRpHq4rcyeoq6vkWLEorfIsJiimpmWeritypqxomWnlnqstdOepaCdnJZ6s8HIq6xmppFiu6i7zaBloaydoQ%3D%3D